Timu kuifuata Green Buffaloes jijini Marrakech kesho

Kikosi chetu kitaondoka kesho saa tatu asubuhi kuelekea Marrakech ambapo mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Green Buffaloes kutoka Zambia utafanyika.

Mechi zetu mbili za mwanzo dhidi ya ASFAR FC na Determine Girls zimefanyika hapa katika mji wa Rabat lakini huu wa mwisho utafanyika Marrakech.

Mchezo wetu dhidi ya Green Buffaloes utapigwa Jumamosi Novemba 5, saa nne usiku kwa saa za nyumbani Tanzania.

Safari ya kutoka Rabat mpaka Marrakech inachukua saa tatu ambapo baada ya kufika wachezaji watapumzika kabla ya kufanya mazoezi ya mwisho.

Tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali ambayo ni moja ya malengo tuliyojiwekea.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER