Timu kuelekea Zanzibar kesho kutetea taji lake

 

Kikosi cha wachezaji 30 kitaondoka kesho mchana kwa boti kuelekea Visiwani Zanzibar tayari kwa Michuano ya Mapinduzi.

Tutaanza harakati za kutetea taji letu kwa kucheza na Mlandege katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Amani, Januari 3 saa 2:15 usiku.

Meneja wa timu Patrick Rweyemamu, amesema tunakwenda Zanzibar kwa lengo moja la kuhakikisha tunapambana na kutetea ubingwa wetu.

Amesema tunayapa umuhimu mkubwa mashindano hayo kwa kuwa tunadumisha Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani.

“Tutaondoka kesho mchana na kikosi kamili cha wachezaji 30 kwa kuwa tunahitaji kuchukua taji hili kwa mara ya pili mfufulizo.

“Tunaipa umuhimu na thamani kubwa michuano hii kwa kuwa ina heshima kubwa katika Muungano na tutaingia kwa lengo moja la kutafuta ubingwa,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER