Timu kuelekea Dubai kesho kwa kambi ya wiki moja

 

Kikosi chetu kinatarajia kusafiri kesho kuelekea Dubai kikiwa na msafara wa watu 38 kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya siku saba kujiandaa na mechi za ligi kuu na mashindano mengine.

Kambi hiyo ni mualiko kutoka kwa Rais wa heshima wa klabu yetu Mohammed Dewji (Mo) ili kuipa nafasi timu ya kufanya maandalizi ya kujiandaa na michuano ligi ya Mabingwa Afrika.

Kambi hiyo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi pamoja na kumpa mwalimu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ nafasi ya kuwafahamu wachezaji wake kwa utulivu.

Tukiwa Dubai tunatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ambapo ratiba kamili itajulishwa baadaye.

Kikosi kitarejea nchini Januari, 14 na moja kwa moja tutaelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Januari 17 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumzia kambi hiyo Robertinho amesema ni maamuzi sahihi ambayo yatampa nafasi ya kuangalia kikosi chake kwa mapana na kuanza kupandikiza falsafa zake akishirikiana na makocha wenzake Juma Mgunda na Selemani Matola.

“Ni uamuzi mzuri kwa Uongozi kunipa muda wa kufanya mazoezi na kikosi kwa utulivu ili kuniwezesha kuwajua wachezaji nakuwapa mbinu zangu,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER