TAARIFA KWA UMMA

Klabu ya Simba imeridhia ombi la aliyekuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes da Rosa la kuachana na Simba kuanzia leo tarehe 26.10.2021

Baada ya tathmini na majadiano ya kina, pande zote zimeafikiana kwa mujibu wa mkataba na manufaa ya wote.

Kutokana na hatua hiyo, aliyekuwa Kocha Msaidizi Thierry Hitimana, ndiye atakuwa Kocha Mkuu wa Simba katika kipindi hiki cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.

Aidha, Klabu pia imefanya mabadiliko madogo katika benchi la ufundi kwa kusitisha mikataba ya aliyekuwa Kocha wa Makipa, Milton Nienov na Kocha wa Viungo, Adel Zrane.

Klabu ya Simba inamshukuru Kocha Gomes na wenzake kwa mafanikio waliyopata katika kipindi walichoitumikia Simba na kuwatakia heri katika majukumu yao mengine huko waendako.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER