TAARIFA KWA UMMA.

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo ( Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Simba Nguvu Moja.

Imani J. Kajula
Afisa Mtendaji Mkuu
Simba Sports Club
07 Novemba 2023

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER