TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na wachezaji wetu watatu wakimataifa, Medie Kagere, Chris Mugalu na Taddeo Lwanga.

Baada ya mazungumzo na wachezaji hao hatimae tumefikia makubaliano ya kuvunja mkataba kwa kuzingatia maslahi ya pande zote.

Uongozi wa Simba unatambua na kuthamini mchango wa wachezaji hao kwa muda wote waliokuwa na kikosi chetu.

Kwa dhati kabisa tunajivunia huduma ya miaka mitano ya Meddie Kagere ambayo ameisaidia klabu yetu kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara nne mfululizo, na kutuwezesha kucheza robo fainali tatu za michuano ya Afrika

Vilevile tunajivunia utumishi uliotukuka wa mshambuliaji wetu Chriss Mugalu ambae kwa wakati wa miaka miwili ametusaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu na ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam Sports pamoja na kutufikisha robo fainali ya michuano ya Afrika

Na kwa upekee kabisa tunamshukuru Taddeo Lwanga ambae nae amekua chachu ya mafanikio kwa klabu yetu kwa muda wa miaka miwili aliyokua nasi

Uongozi wa Simba unawatakia kila la heri wachezaji hao katika maisha yao mapya ya mpira wa miguu

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER