Steven Mukwala ni Mnyama

Mshambuliaji Steven Mukwala raia wa Uganda amejiunga nasi baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kutoka Asante Kotoko ya Ghana.

Mukwala mwenye umri wa miaka 24 ni mshambuliaji kinara mwenye uwezo wa kufunga tunategemea atakuwa msaada mkubwa kwa timu.

Mukwala amefunga mabao 14 na kuisaidia kupatikana kwa mengine mawili katika michezo 28 katika ligi kuu ya Ghana

Mukwala ana urefu wa futi 5.9 na ana uwezo wa kufunga magoli ya aina yeyote lakini pia ni mzuri kwenye mipira ya juu na mipira ya krosi na pia hivyo anatarajiwa atakuwa msaada mkubwa kwa timu yetu.

Moja ya eneo ambalo lilikuwa na mapungufu msimu uliopita ni katika safu ya ushambuliaji na ujio wa Mukwala utaongeza uimara wa timu akisaidiana na Fredy Michael.

Mukwala amewahi kuzitumikia timu za Vipers FC, Maroons FC zote za Uganda kabla ya kutimkia Asante Kotoko ya Ghana.

Tunaendelea kufanya usajili kwa umakini mkubwa na kuimarisha kikosi chetu katika idara zote ili msimu ukianza tuwe kwenye ubora mkubwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER