Wapinzani wetu St. George ambao tutacheza nao mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye kilele cha Simba Day wamewasili jijini Dar es Salaam leo na msafara wa watu 45.
Mabingwa hao mara 29 wa Ethiopia wamefikia katika Hotel ya Sea Cape Mbezi Beach ambapo kesho watafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mtanange wa Jumatatu.
Tumewaalika St. George kwenye tamasha letu la mwaka huu kwa kuwa tunajua uwezo wao na watatupa kipimo kizuri kuelekea msimu ujao.
Kila mwaka tumekuwa na utaratibu wa kualika timu bora kwenye kilele cha Simba Day kwa ajili ya kukipima kikosi chetu.