Sportpesa yatoa mamilioni kufika robo fainali Shirikisho

Wadhamini wetu wakuu kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa imetupatia kitita cha Sh milioni 50 (50,000,000) kwa kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mujibu wa makubaliano ya kimkataba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Sportpesa, Tarimba Abbas ametupongeza kwa mafanikio tuliyopata kwa miaka minne ambayo tumefanya vizuri katika ligi ya ndani na michuano ya kimataifa.

Tarimba amesema miaka minne iliyopita Simba haikuwa katika hali hii ni tofauti na ilivyokuwa kwa hiyo anaamini tuna mchango mkubwa kwenye mafanikio yao.

“Hii ni mara ya nne kuwakaribisha Simba katika ofisi zetu kwa shughuli kama hii. Katika mkataba wetu kuna makabaliano ambayo wanapofikia hatua fulani kuna ‘bonus’ wanapata na leo tumekamilisha.

“Kwa upande wa ligi Simba imechukua bonus ya Sh milioni 100 kila mwaka na tunawapongeza kwa hilo wametutungaza vizuri na matumaini yetu tutasaini mkataba mpya baada ya huu kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu,” amesema Tarimba.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez ameishukuru Sportpesa kwa kufuata makubaliano ya mkataba na amekiri kuwa anaamini baada ya mazungumzo kukamilika tutasaini mkataba mpya.

“Kwa niaba ya klabu ya Simba tunawashukuru Sportpesa kwa kufuata makubaliano ya mkataba kwa kutoa bonus hii ya Sh 50,000,000 sisi tutaendelea kufanya vizuri na kuchukua tena na tena bonus hizi,” amesema Barbara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER