Sisi haooo Fainali Mapinduzi kibabe

Kikosi chetu kimetinga Fainali ya Michuano ya Mapinduzi kwa kishindo baada ya kuifunga Namungo FC mabao 2-0 mchezo uliopigwa Uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.

Medie Kagere alitupatia bao la kwanza dakika ya 15 baada ya shuti lililopigwa na Pape Sakho kuokolewa na mlinda mlango wa Namungo, Jonathan Nahimana kabla ya kumkuta mfungaji.

Baada ya bao hilo tuliendelea kumiliki mpira na kutengeneza nafasi huku Namungo wakicheza na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Sakho alitupatia bao la pili dakika ya 48 baada ya kuwapiga chenga walinzi wa Namungo kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Kagere.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Sakho, Kagere na Rally Bwalya, Kibu Denis na Sadio Kanoute na kuwaingiza Hassan Dilunga, John Bocco, Mzamiru Yassin, Bernard Morrison na Etop Udoh.

Katika fainali tutakutana na Azam FC ambayo imetangulia baada ya kuifunga Yanga SC mabao 9-8.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER