Simba yazitaka pointi tatu za Azam Kesho

Pamoja na kutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara lakini tunahitaji kushinda mechi zetu zote mbili zilizobaki ikiwepo ya kesho dhidi ya Azam FC.

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union juzi tulitawazwa Mabingwa wa Ligi Kuu 2020/21 kwa mara ya nne mfululizo.

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema timu itaingia uwanjani kwa lengo la kutafuta pointi tatu na hatutaichukulia poa baada ya kutangazwa mabingwa.

“Ni kweli tumeshinda ubingwa wa ligi lakini haimaanishi tunazichukulia kawaida mechi zilizobaki. Mechi dhidi ya Azam itakuwa ngumu lakini tupo tayari kupambana kupata ushindi,” amesema Matola.

Matola amewataja nyota wanne Bernard Morrison, Jonas Mkude, Miraji Athumani na Ibrahim Ajibu ambao watakosekana kwenye mchezo wa kesho kwa sababu tofauti.

“Tutawakosa Morrison ambaye ameenda nchini kwao Ghana ana matatizo ya kifamilia, Mkude suala lake bado halijamalizika, Miraji amepata majeruhi mazoezini na Ibrahim Ajibu,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER