Simba yazidi kujinoa ikiisubiri Coastal Union

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jumapili saa moja usiku.

Baada ya mchezo wetu wa Jumatano dhidi ya Polisi Tanzania kikosi chetu kiliingia kambini moja kwa moja tayari kwa maandalizi ya mechi hii.

Ushindi tuliyopata dhidi ya Polisi umeongeza morali kwa wachezaji ambapo wamehakikisha wanapambana tunaibuka na ushindi mwingine Jumapili.

Kwa sasa tunajipanga kuhakikisha tunashinda katika kila mchezo ili kurudisha hali ya kujiamini kwa wachezaji na kuendeleza mbio za kutetea taji letu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER