Simba yatua salama Songea, yapata mapokezi ya kifalme

Kikosi chetu kimewasili salama mjini Songea na kupata mapokezi ya kifalme kutoka kwa idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza kutulaki na kutupa hamasa.

Timu iko Songea kwa ajili mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumamosi Juni 26, katika Uwanja wa Majimaji saa tisa alasiri.

Wachezaji wote waliosafiri wako vizuri kiafya tayari kwa mchezo huo ambapo utatupa tiketi ya kucheza fainali kama tutaibuka na ushindi.

Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amewataja wachezaji ambao hawajasafiri na timu kuwa ni Ibrahim Ajibu, Chris Mugalu ambao ni majeruhi huku Jonas Mkude suala lake la nidhamu likiwa halijamalizika.

“Timu imefika salama Songea na tunashukuru mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuja kutulaki na kuwafanya wachezaji wajione wana deni kubwa kuelekea mchezo wa Jumamosi,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER