Simba yatoa zawadi ya Christmas kwa mashabiki

Kikosi chetu kimetoa zawadi ya Christmas kwa wapenzi na mashabiki wetu ndivyo unavyoweza kusema baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Katika mchezo huo, Mohamed Hussein alitupatia bao la kwanza dakika ya 10 kwa shuti kali la mguu wa kushoto ndani ya sita baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jonas Mkude.

Dakika mbili baadaye Joash Onyango alitufungia bao la pili kwa kichwa baada ya kumaliza mpira wa kona uliopigwa na Rally Bwalya.

Abdul Hillary aliwapatia KMC bao la kwanza dakika ya 39 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Emmanuel Mvuyekure.

Kibu Denis alitupatia bao la tatu dakika ya 46 kwa shuti la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Shomari Kapombe kuzuiwa na mlinzi Ismail Gambo kabla ya kumkuta mfungaji.

Dakika ya 57 Kibu alitufungia bao la nne kwa shuti kali la mguu wa kuahoto nje ya 18 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Mkude.

Kocha Pablo Franco alifanya mabadiliko tofauti kwa akiwatoa Bwalya, Pape Sakho, Kibu na Mohamed Hussein na kuwaingiza Yusuf Mhilu, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwinuke, na AbdulSamad Kassim.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER