Simba yatoa msaada Gereza la Wanawake Segerea

Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation imetembelea Gereza la Wanawake la Segerea na kutoa misaada mbalimbali katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Klabu yetu imekuwa na utaratibu wa kutoa misaada kwa jamii na wenye uhitaji kama vituo vya watoto yatima, hospitalini na leo tumetembelea magereza.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema tumekuwa tukigusa maisha ya watu kwa namna moja au nyingine na ndicho kinachotusukuma kutoa misaada mbalimbali kwa jamii.

Barbara amesema kwa kuwa leo ni Siku ya Wanawake Duniani tumeona itakuwa vizuri kuja kutoa misaada kwa wafungwa Wanawake ili nao wajione wanathaminiwa na jamii.

“Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation tumekuja katika Gereza la Wanawake la Segerea na kutoa misaada mbalimbali kama tunavyofanya kila mwaka.

“Tumekuwa tukifanya hivi kila mwaka. Mwaka jana tulitembelea vituo vya watotao yatima na kutoa misaada mbalimbali lakini leo tumewakumbuka wenzetu wa Segerea,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Mrakibu wa Magereza, Yunge Saganda umeushukuru uongozi wa Klabu kwa msaada uliotoa huku akiziomba taasisi nyingine ziendelee kuiga mfano huo.

“Wafungwa wametengwa na jamii lakini wanahitaji huduma za kijamii kama wengine, kwa dhati niupongeze uongozi wa Simba kwa misaada hii na nawaomba wakati mwingine mkipata nafasi mje tena,” amesema SP Saganda.

Katika tukio hilo, Uongozi wa kKabu umeambatana na timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER