Simba yatoa milioni 10 Mwananyamala wadi ya mama na mtoto

Uongozi wa Klabu ya Simba umetoa cha Sh milioni 10 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto.

Simba imetoa kiasi hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Simba Day, Septemba 19 kama ada kila mwaka hutoa kwa jamii yenye uhitaji.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema mwaka huu tumeamua kutoa fedha badala ya vitu ili kutoa wigo kwa uongozi wa Hospitali kununua vitu ambavyo vinahitajika kwa haraka.

“Uongozi ndiyo unajua kitu gani kinahitajika kwa haraka na kiasi cha fedha tulichotoa kitasaidia sehemu fulani ingawa tunajua hakitaweza kumaliza kabisa tatizo,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Katibu wa Hospitali, Lilian Mwanga ameupongeza uongozi wa klabu kwa msaada huku akiutaka uhusiano huo kuendelea na usiishie leo na kwamba fedha hizo zotatumika kama ilivyokusudiwa.

“Kwa niaba ya Uongozi wa Hospitali naipongeza Simba kwa msaada huu, mnaweza kuuona kama ni mdogo lakini kwetu ni mkubwa na tutaenda kuutumia kama ilivyokusudiwa na tunawakaribisha wakati mwingine,” amesema Lilian.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER