Simba yatoa 12 timu za taifa, watatu mkopo

Jumla ya wachezaji 12 wa timu ya Simba wameitwa katika timu mbalimbali za taifa barani Afrika kwa ajili ya michuano ya kuwania kufuzu kwa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Kati ya wachezaji hao, wachezaji wanane wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na wengine wameitwa katika vikosi vya Uganda, Rwanda na Zimbabwe. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Mohamed Hussein, Israel Mwenda, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Kennedy Juma, John Bocco na Muzamiru Yassin ambao wote wameitwa Taifa Stars.

Wengine ni Perfect Chikwende (Zimbabwe), Taddeo Lwanga (Uganda) na Meddie Kagere (Rwanda). Wachezaji hao tayari wameondoka kambini Morocco ambako Simba imekwenda kujiandaa na msimu ujao wa mashindano na wameungana na wengine ambao wameondoka kwa sababu tofauti.

Wachezaji Ibrahim Ame amerejea kujiunga kwa mkopo na timu ya Mtibwa ya Morogoro huku David Kameta akijiunga na Biashara United ya Mara kwa mkopo pia. Mlinda mlango Benno Kakolanya alirejea nchini baada ya kufiwa na mama yake mzazi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER