Simba yatinga robo fainali ASFC

Kikosi chetu kimeingia robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Kagera walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 45 lililofungwa na Erick Mwijage kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kulia Dickson Mhilu.

Bernard Morrison alitusawazishia bao hilo dakika ya 55 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Luis Miquissone kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na John Bocco.

Kinara Medie Kagere alitufungia bao la pili dakika ya 67 baada ya kupokea pasi ya Morrison aliyemzidi ujanja mlinzi mmoja wa Kagera.

Kocha Didier Gomez aliwatoa Taddeo Lwanga, Rally Bwalya na Kagere nafasi zao zikachukuliwa na Morrison, Bocco na Erasto Nyoni.

Tumeingia robo fainali tukiwa kumbukumbu ya kutwaa ubingwa wa michuano hii huku tukiwa na nafasi ya kufanya hivyo tena msimu huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER