Simba yatimiza lengo, yatwaa ubingwa wa FA

Timu yetu imetawazwa mabingwa wa Michuano Azam Sports Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Yanga katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika hapa Kigoma.

Ubingwa huu ni sehemu ya malengo tuliokuwa tumejiwekea kabla ya kuanza msimu kuhakikisha tunatetea ubingwa wa michuano hii pamoja na wa Ligi Kuu ya Vodacom ambao tulifanikiwa kuutetea.

Mchezo ulianza taratibu timu zikisomana huku mchezo ukichezwa zaidi eneo la katikati ya uwanja mashambulizi yakiwa machache.

Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe alitolewa baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45 kipindi cha kwanza baada ya kumpiga kiwiko Nahodha John Bocco.

Kipindi cha pili tuliongeza mashambulizi na kuliandama lango la Yanga kwa kutengeneza nafasi ingawa changamoto ikawa ni kwenye kuzitumia.

Dakika ya 77 kiungo Taddeo Lwanga alitufungia bao hilo pekee kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Luis Miquissone.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Rally Bwalya, Clatous Chama na Chris Mugalu na kuwaingiza Bernard Morrison, Erasto Nyoni na Kennedy Juma.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER