Simba yateuliwa kuwa Balozi wa Utalii Zanzibar.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Mohammed Said ameiteua klabu yetu ya Simba kuwa Balozi wa Utalii wa Zanzibar.

Waziri Simai amechukua uamuzi huo kwa kutambua mchango mkubwa klabu yetu katika kutangaza utalii wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Klabu ya Simba ilianzisha mkakati wa kuitangaza Zanzibar kupitia kauli mbiu ya Visit Zanzibar katika jezi na mitandao yetu ya kijamii wakati huu wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Akizungumza kwa niaba ya klabu ya Simba Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amsema,“ tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutambua mchango wa timu yetu kutangaza utalii hivyo kukuza uchumi, tunaona fahari kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER