Simba yatawala Tuzo za Ligi Kuu 2020/2021

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo limetangaza utoaji wa tuzo mbalimbali katika mashindano yote ya msimu wa 2020/21 huku timu yetu ikitawala kwa karibu kila kipengele.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Oktoba 21.

Kocha wetu mkuu Didier Gomes ambaye ametuwezesha kutwaa ubingwa msimu uliopita anawania tuzo ya kocha bora wa msimu.

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wetu Clatous Chama na nahodha wetu John Bocco wanawania tuzo ya mchezaji bora wa msimu.

Walinzi wetu Mohamed Hussein na Shomari Kapombe wanawania tuzo ya beki bora wa msimu kutokana na uwezo walioonyesha msimu uliopita.

Mlinda mlango wetu Aishi Manula anawania tuzo ya kipa bora wa msimu ambayo ameitwaa mara nne mfululizo.

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wetu Luis Miquissone pamoja na nahodha Bocco wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Azam Sports Federation Cup.

Pia timu yetu inawania tuzo ya timu yenye nidhamu ya msimu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER