Simba yatanguliza mguu mmoja ndani makundi Shirikisho Afrika

Ushindi wa mabao 3-0 tuliopata nyumbani dhidi ya Red Arrows leo umetufanya kuingiza mguu mmoja ndani katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Matokeo ya leo yametupa mtaji mzuri wa mabao ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Desemba 5 nchini Zambia.

Katika mchezo wa leo, Bernard Morrison alitufungia bao la kwanza dakika ya 17 kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni nje kidogo ya 18.

Medie Kagere alitupatia bao la pili dakika tatu baadaye baada ya Morrison kuwapiga chenga walinzi wa Red Arrows.

Dakika ya 31 Morrison alikosa mkwaju wa penati uliopanguliwa na mlinda mlango wa Red Arrows baada ya Hassan Dilunga kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Dakika ya 77 Morrison alitupia la tatu baada ya kuwapiga chenga walinzi wa Red Arrows na kupiga shuti la chini chini ambalo mlinda mlango alidhani unatoka.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Pascal Wawa, Sadio Kanoute, Dilunga, Kagere na Rally Bwalya na kuwaingiza Henock Inonga, Mzamiru, Ibrahim Ajibu, John Bocco na Peter Banda.

SHARE :
Facebook
Twitter

4 Responses

  1. Paragraph writing is also a fun, if you be familiar with after that you can write or else it is complicated to
    write.

  2. Hey there! I simply want to give you a huge thumbs up for your great information you have here on this post.
    I am returning to your website for more soon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER