Klabu yetu imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Malawi, Duncan Nyoni kutoka Timu ya Silver Strikers FC.
Duncan 23, ambaye hutumia zaidi mguu wa kushoto pia ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Malawi ‘The Flames’.
Duncan ni mchezaji mwenye umbo kubwa na anaweza kucheza nafasi mbalimbali za eneo la ushambuliaji lakini amekuwa akitumika zaidi kama winga wa kushoto.
Duncan anakuwa mchezaji wa pili raia wa Malawi kujiunga nasi msimu huu baada ya Peter Banda kutoka Big Bullets kufanya hivyo wiki iliyopata.
Tayari tumekamilisha usajili wa wachezaji watatu ambao ni Banda, Yusuph Mhilu na Duncan.
One Response
Nguvu moja mnafanya sajili za vijana wenye uwezo kwa lengo la kuitumikia timu kwa mda mrefu