Simba yashusha kocha wa viungo kutoka Hispania

Klabu yetu imefanikiwa kumpata kocha mpya wa viungo, Daniel De Castro Rayes raia Hispania ambaye anakuja kuongeza nguvu katika benchi la ufundi.

De Castro anaungana na Kocha Mkuu Pablo Franco aliyetua nchini wiki iliyopita ambaye naye ametoka Hispania.

Msimu wa 2020/21 De Castro alikuwa Kocha Msaidizi wa Viungo wa Timu ya Politehnica Ias ya Romania.

Msimu wa 2019/20 De Castro alikuwa kocha msaidizi wa viungo wa timu ya Rapid Bucharest ya Romania pia.

Msimu wa 2018/19 De Castro alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Real Madrid ya vijana chini ya miaka 18 ambayo ilitwaa ubingwa wa Hispania.

ELIMU

Kocha De Castro ana Shahada ya Mafunzo ya Utimamu wa Mwili Katika Soka aliyopata mwaka 2018/19 Chuo cha Madrid

Pia amefanya kozi ya mafunzo ya uchambuzi wa viwango katika soka kutoka Chuo kikuu cha Polytechnic Madrid mwaka 2018.

Ana Stashahada ya Utaalamu wa Elimu ya Mwili (UEFA – A ) aliyopata katika chuo cha Laguna nchini Hispania mwaka 2010.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER