Simba yasaini mkataba wa bilioni mbili na Vunjabei

Klabu ya Simba imeisaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Vunjabeigroup wa kutengeneza na kusambaza jezi za timu ya wakubwa, wanawake na vijana wenye thamani ya Sh bilioni mbili.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema kampuni 11 ziliomba tenda hiyo lakini Vunjabeigrouo ametimiza vigezo vilivyowekwa ndiyo maana tumesaini mkataba huo.

Amesema licha ya kutengeneza jezi, kampuni ya Vunjabeigroup pia watatengeza vifaa kama barakoa, makasha ya simu, mabegi, miwani na kofia ambazo zitakuwa na nembo za Klabu ya Simba.

“Leo ni rasmi tumesaini makubaliano hayo ya miaka miwili na Vunjabeigroup kushinda tenda na kuzipiku kampuni nyingine 11.

“Tunategemea mkataba wetu utakwenda sawa na makubaliano kwani tunaamini Vunjabeigroup ni kampuni kubwa iliyobobea katika uuzaji nguo,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vunjabei Group, Fred Fabian maarufu Fred Vunjabei ameushukuru uongozi wa klabu yetu kwa kufuata weledi katika tenda na kutoa haki kwa mshindi kufuatia kushindanishwa na makampuni makubwa.

Fred ameongeza kuwa anaamini atapata faida kubwa kutokana na ‘brand’ iliyopo Simba ambapo amekiri ni mkataba mkubwa waliosaini tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo.

“Naushukuru uongozi wa Klabu ya Simba kwa kutuamini na kutupa nafasi hii, sisi ni kampuni ndogo na tumeshindana na kampuni kubwa kutoka nje ya nchi lakini nafasi imetuangukia sisi kutokana na Klabu kufuata weledi.

“Katika usambazaji wetu, tutakuwa na duka na gari maalumu kwa ajili ya kuuza jezi na tutatembea kila sehemu ambayo timu itakuwepo kikubwa ni kuhakikisha kila Mwanasimba anapata jezi halisi ya Simba,” amesema Fred Vunjabei.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER