Kikosi chetu leo asubuhi kimefanya mazoezi gym kuendelea kutafuta stamina kabla ya kuanza mikiki mikiki ya msimu mpya wa ligi 2021/22.
Baada ya kikosi kutua hapa Morocco wiki mbili zilizopita kilianza mazoezi ya gym kabla ya kuelekea uwanjani kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali.
Juzi Jumamosi tulicheza mechi ya kirafiki dhidi ya FAR Rabat hivyo benchi la ufundi limeona tunahitaji kurudi Gym ili kuongeza stamina.
Wachezaji wanajitahidi kujituma mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi msimu utakapoanza.
Aidha, wachezaji wapya tuliowasajili nao wameendelea kuonyesha uwezo mkubwa huku wakionekana kuwazoea wenzao haraka.