Simba yarejea mazoezini Mo Arena

Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi ijayo.

Timu ilipoerejea kutoka jijini Arusha wakati wa maandalizi ya Simba Day kikosi kilifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans kutokana na viwanja vyetu kuwa kwenye ukarabati.

Wachezaji wote tuliowasajili wamehudhuria mazoezi na wako tayari kwa mchezo huo mkubwa wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi 2021/22.

Meneja wa timu Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na hakuna majeruhi kitu ambacho kinalifanya benchi la ufundi kuwa na uwiano mpana wa kupanga programu za mazoezi.

“Kikosi kimefanya mazoezi jioni kujiandaa na mchezo ujao wa Ngao ya Jamii na kimeingia kambini moja kwa moja,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER