Simba yarejea kwa kishindo VPL, yaipiga Mtibwa ‘mkono’

Kikosi chetu kimeonyesha dhamira ya kutaka Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuichakaza bila huruma Mtibwa Sugar mabao 5-0.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo ushindi huo unatafanya kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kufikisha pointi 49 alama mbili nyuma ya anayeongoza huku tukiwa na mechi tatu mkononi.

Mchezo huo uliokuwa na mvuto wa aina yake, ulianza safari ya karamu ya magoli baada ya Clatous Chama kutupatia bao la kwanza dakika ya tisa kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja nje kidogo ya 18.

Rally Bwalya aliongeza bao la pili dakika ya 19 baada ya kupokea pasi ya Shomari Kapombe akiwa ndani ya kisanduku na kumpiga chenga mlinzi mmoja wa Mtibwa kabla ya kuweka mpira kambani.

Tulienda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0 baada ya Kagere kuongeza jingine dakika ya 43 akimalizia pasi iliyopigwa na Bwalya.

Kagere aliongeza bao la nne dakika ya 51 kabla ya Luis Miquissone kutupia la tano dakika ya 68 akimalizia pasi ya kisigino iliyopigwa na Chama.

Kocha Didier Gomez aliwatoa Erasto Nyoni, Miquissone na Pascal Wawa nafasi zao zikachukuliwa na Perfect Chikwende, John Bocco na Kennedy Juma.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER