Kikosi chetu kimerejea jijini Dar es Salaam kutoka jijini Mwanza leo na kuingia moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Mbeya City.
Jana tulicheza na Polisi Tanzania katika Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushindi wa bao moja ambalo lilifungwa na Luis Miquissone kwa mpira wa adhabu.
Jumanne Juni 22, kikosi kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Mbeya City katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambayo inaelekea ukingoni.
Meneja wa timu Patrick Rweyemamu amesema baada ya mchezo wa Jumanne kikosi kitaelekea Songea kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya michuano ya FA dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Majimaji.