Simba yarejea Dar wachezaji wapewa mapumziko

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam leo asubuhi kikitokea Mtwara ambapo wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja.

Baada ya mchezo dhidi ya Namungo juzi kikosi kilirejea Mtwara usiku ule ule na jana jioni kilifanya mazoezi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona kurejesha utimamu wa mwili kwa wachezaji (recovery).

Baada ya mapumziko ya siku moja kesho kikosi kitasafiri kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Juni 3, mwaka huu.

Sisi ndio vinara wa Ligi Kuu tukiwa na alama 64 baada ya kucheza mechi 26 tukiwa na michezo mitatu mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. HONGERENI SANA CLUB NZIMA KWA UJUMLA KWA MWENENDO WA TEAM NZIMA BENCHI LA UFUNDI NA UONGOZI WOTE KWA UJUMLA, SISI MASHABIKI TUNAFURAHI SANA KWA BURUDANI MURUA MNAYOTUPATIA UWANJANI LKN PIA NJE YA UWANJA TUNATEGEMEA MAKUBWA ZAIDI YA HAYA TUYAONAYO IKIWA NI PAMOJA NA KUTWAA MAKOMBE HAYO MAWILI YA HAPA NYUMBANI..NAWATAKIA AFYA NJEMA NA MUNGU AWABARIKI.
    #NGUVUMOJA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER