Simba yarejea Dar, wachezaji wapewa mapumziko

Kikosi chetu kimewasili jijini Dar es Salaam salama mchana huu kutoka Mwanza na wachezaji wamepewa mapumziko huku wale walioitwa na timu zao za taifa wakiruhusiwa kwenda kujiunga nazo.

Jana kikosi chetu kilikuwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa sasa ligi imesimama kupisha mechi za kirafiki za kimataifa za timu ya Taifa ambayo itachukua wiki mbili kabla ya kurejea na kumalizia mechi zilizobaki.

Hadi ligi inasimama sisi ndiyo vinara tukiwa na pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 huku tukiwa na michezo miwili mkononi.

Mchezo wetu wa kwanza ligi ikirejea utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba Juni 19, mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER