Simba yapoteza Ugenini

Kikosi chetu kimepoteza kwa mabao 4-0 mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs uliopigwa katika Uwanja wa FNB jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tukiwa tuna kazi kubwa ya kufanya kuvuka hatua hii.

Kipigo hiki kinatufanya kuhitaji kupata ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Mei 22 ili kutinga nusu Fainali.

Wenyeji Kaizer walipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa mlinzi Mathoho Erick kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Nahodha Bernard Parker.

Mshambuliaji Nurkovic Samir aliipatia Kaizer bao la pili kwa kichwa tena dakika ya 33 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Manyama Lebogang.

Nurkovic aliwapatia Kaizer bao tatu dakika ya 57 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupata mpira kutoka kwa Mohamed Hussein ambaye alitaka kuondoa hatari.

Castro Leonardo aliipatia Kaizer bao la nne kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Manyama kutoka upande wa kulia.

Kipindi cha pili Kocha Didier Gomes aliwatoa Jonas Mkude, Rally Bwalya na Luis Miquissone na kuwaingiza Medie Kagere, Hassan Dilunga na John Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER