Simba yapiga tizi Nyamagana kuiwinda Ruvu Shooting

Kikosi chetu kimefanya mazoezi leo jioni kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba keshokutwa Alhamisi.

Kikosi kiliwasili hapa jijini Mwanza saa tano asubuhi na wachezaji walipumzika kwa saa chache kabla ya jioni kwenda mazoezini.

Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wote 21 waliosafiri na kikosi wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa Ruvu Shooting.

Rweyemamu amesema benchi la ufundi na wachezaji wanafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.

Leave a comment