Simba yapiga bonge la ‘Come Back’ yavunja mwiko Majaliwa Stadium

Kikosi chetu kimeibuka na ushindi wa ‘Come Back’ wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC na kuvunja mwiko wa kushindwa kupata ushindi kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Kabla ya mchezo wa leo tulikuwa hatujawahi kushinda wala kupata bao kwenye uwanja huo.

Wenyeji Namungo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 22 kupitia kwa Nzigamasabo Steve baada ya kupokea pasi kutoka mshambuliaji Ralient Lusajo.

Baada ya bao hilo tuliliandama lango la Namungo kutafuta bao la kusawazisha huku tukitengeza nafasi ambazo hata hivyo hazikufanikiwa kipindi cha kwanza.

Chris Mugalu alitusawazishia bao hilo dakika ya 78 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe kufuatia pasi ndefu ya mpenyezo kutoka kwa Hassan Dilunga.

Dakika ya 84 Nahodha John Bocco alitufungia bao la pili kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mugalu.

Bernard Morrison alifunga bao la tatu dakika ya 87 kwa shuti kali lililotinga moja kwa moja wavuni baada kumchungulia mlinda mlango Jonathan Nahimana aliyekuwa ametoka kidogo nje eneo lake

Kocha Didier Gomes aliwatoa Mzamiru Yassin, Medie Kagere na Rally Bwalya na kuwaingiza Morrison, Bocco na Hassan Dilunga.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Hakika Simba ni next level kwa sasa, timu inajua kupambania matokeo. Namungo pamoja na utopolo wamefurahia kwa dk karbu 75, afu baada ya hapo huzuni na kilio kikafuata. Mnyama 🦁🦁🦁 akawa anatabasamu 💪💪💪.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER