Simba yapewa Kaizer Chiefs Mabingwa Afrika

Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali imetoka leo ambapo tumepangwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Johannesburg kati ya Aprili 14/15 kabla ya kurudiana jijini Dar es Salaam wiki mbili baadae.

Katika hatua ya makundi tuliibuka kinara wa kundi wa A dhidi ya miamba ya soka Afrika, Al Ahly, El Merrikh na AS Vita.

Kwenye mechi sita za hatua ya makundi tulishinda nne tukatoka sare mechi moja na kupoteza moja na kufanikiwa kukusanya alama 13.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Jaman mm kama shabiki wa simba naomba wachezaji mashabiki na benchi la ufundi tusije kuidharau kaizer chief maan hata kama ni timu ndogo ila pia inamalengo yake… Ili kutimiza malengo yake lazima wajipange kwahiyo lazima kazier atakuwa amejipanga tusiende kifua mbele kama sisi ni bora hapana tuchukulie nikama mechi nyingine na tucheze kwa kuwasoma ili tuweze kupata point…. #Simba nguvu moja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER