Simba yapata alama muhimu ugenini

Timu yetu ya Simba SC, leo imeendelea kubaki kileleni mwa Kundi A baada ya kupata alama moja muhimu iliyotokana na sare ya bila kufungana dhidi ya Al Merreikh kwenye mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama saba ambazo haziwezi kufikiwa na Al Ahly na AS Vita wenye alama tatu kila mmoja.

Katika mchezo wa leo, hatukutengeneza nafasi nyingi kama kawaida yetu ingawa tulimiliki sehemu kubwa ya mechi kwenye kila kipindi.

Katika mchezo wa leo, Kocha Didier Gomez aliwatoa Mzamiru Yassin, Rally Bwalya, Clatous Chama na Chris Mugalu nafasi zao zikachukuliwa na Erasto Nyoni, Hassan Dilunga, Francis Kahata na Medie Kagere.

Machi 16 tutacheza mechi ya marudinano na Al Merreikh katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER