Simba yapaa kuelekea Morocco kwa ‘Pre Season’

Kikosi chetu kimeondoka nchini mchana huu kuelekea Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22 (Pre Season) kikiwa na wachezaji 24.

Kambi hiyo itakuwa ya wiki mbili na timu itarejea nchini kwa ajili ya kumalizia maandalizi kabla ya kuanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi kuu mwishoni mwa Septemba.

Tumeamua kwenda kuweka kambi nchini Morocco kwa kuwa tunafahamu tutapata utulivu na kuwaweka wachezaji wetu vizuri kabla ya kuanza msimu.

Baada ya timu kurejea, kutakuwa na siku chache kabla ya Tamasha kubwa la Simba Day ambapo tutatambulisha wachezaji.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Hongereni sana kwa kusafiri salama chama langu la Simba,lakini kinachonihuzunisha ni tetesi za Chama kutorejea nchini na timu.All on all itakavyokuwa
    all the best Simba 🦁 Sc

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER