Simba yakabidhiwa mamilioni ya Ubingwa 2020/21

Timu yetu imekabidhiwa Sh milioni 100 baada ya kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Msimu wa 2020/21 katika usiku wa Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) 2021 zinazofanyika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni mgeni rasmi na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu, Salum Abdallah ‘Try Again’ na Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez.

Pia timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imekabidhiwa kitita cha Sh milioni 15 baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake ‘Serengeti Lite Premier League’ msimu uliopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER