Simba yajitokeza vipengele vitano tuzo za kidijitali

Kuelekea hafla ya utoaji wa tuzo za Kidijitali zitakazofanyika Desemba 12, jijini Dar es Salaam klabu yetu, viongozi na wafanyakazi wake wamehusishwa katika vipengele vitano.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Programu ya Kidijitali ya Tanzania Digital Awards ambazo zilianza mwaka jana na huu ni mwaka wa pili.

Majina ya watu au taasisi tano ambazo zimeingia fainali katika kinyang’anyiro hicho walipendekezwa na watu kuanzia Oktoba kabla ya kamati maalumu kuwachuja na kuwapitisha ili kupigiwa kura kupitia tovuti ya Tanzania Digital Awards.

Mwekezaji wa klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameiingia kwenye vipengele viwili ambavyo ni chaguo la watu (People’s Choice) upande wa wanaume na Kiongozi wa Biashara Mtandaoni.

Klabu yetu ya Simba ipo katika kipengele cha Timu Bora ya Soka ya Kidijitali wakati Nahodha wetu John Bocco akiwania tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka huku mpiga picha wetu Rabbi Hume akiwania tuzo ya mpiga picha bora wa mwaka.

Ili kuwapigia kura unatakiwa  kuingia kwenye tovuti ya www.digitalawards.co.tz bofya vote now kisha wapigie Wanasimba ili tuibuke kidedea kwenye vipengele vyote.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER