Simba yajipima na Green Warriors

Kikosi chetu leo jioni kimecheza mechi ya kirafiki ya kimazoezi na Green Warriors katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Katika mchezo huo kocha Pablo Franco aliwaanzisha wachezaji ambao hawakucheza dhidi ya Ruvu Shooting ili apate kuwaona wote.

Tulianza mchezo huo kwa kasi huku mabao yetu yote yalipatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa Banda, Duncan na Gadiel.

Kipindi cha pili Kocha Pablo aliwaingiza Pape Sakho, Ally Salim, Ibrahim Ajibu na Israel Patrick, Yusuph Mhilu na kuwatoa Bocco, Erasto, Benno na Bwallya, Kanoute na Banda.

Mhilu alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne na kukamilisha ushindi huo mnono.

Kikosi kilichoanza

Benno Kakolanya (30), Jimmyson Mwinuke (21), Gadiel Michael (2), Henock Inonga (29), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Duncan Nyoni (23), Sadio Kanoute (13), John Bocco (22), Rally Bwalya (8) na Peter Banda (11).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER