Simba yajifua kabla ya kurejea Dar

Kikosi chetu kimefanya mazoezi leo jioni katika Uwanja wa Discovery Soccer Park hapa jijini Johannesburg kujiweka miili sawa kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini.

Baada ya mchezo wa jana wa Robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs wachezaji wanapaswa kufanya mazoezi ili kurejesha miili katika utimamu wake kabla ya kuanza safari.

Uwanja wa Discovery Soccer Park ndiyo tumekuwa tukiutumia tangu tulipowasili hapa Afrika Kusini kutokana na ubora wake.

Kikosi kinatarajia kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam leo usiku kupitia Nairobi.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER