Simba yaja kivingine, kutoka na ‘Mascot’ kila kona

Wadhamini wa Klabu ya Simba, Mo 29 na Mo Extra wamezindua Mascot (Kinyago) rasmi kwa ajili ya timu kijulikanacho kama ‘Mo Rafiki’ ambacho kitakuwa kinapatikana kila sehemu ambapo kikosi kitakuwepo.

Ofisa Masoko wa Kampuni ya Mohamed Enterprises (METL), Fatema Dewji amesema lengo la kuzindua Mascot hiyo ni kuongeza furaha, hamasa na umoja baina ya mashabiki popote ambapo timu itakuwepo.

 “Kuelekea kilele cha Simba Day Jumapili hii katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mascot watakuwa wanazunguka mitaani kuanzia leo kuongeza hamasa ambapo watakuwa wanatoa zawadi kama sabuni, jezi na kujishindia tiketi,’ amesema.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez ameishukuru Kampuni ya METL kwa kuona umuhimu wa kuwa na Mascot kama ilivyo kwa klabu kubwa duniani kama Manchester United na Arsenal.

“Si kwenye Simba Day au mechi za Uwanja wa Benjamin Mkapa bali Mascot atakuwepo kila Simba itakapowepo iwe Bukoba, Mara, Morogoro au popote itakapocheza atakuwepo,” amesema Barbara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER