Simba yaingia kambini kujiandaa na Polisi Tanzania

Kikosi chetu kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Jumatano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Baada ya mchezo wa jana timu imeingia moja kwa moja kujiandaa na mechi hiyo ambayo tunahitaji ushindi ili kurejesha imani kwa mashabiki.

Meneja wa Timu Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na maandalizi yanaendelea lengo ni kukahikisha tunapata alama tatu muhimu.

“Timu imeingia kambini tangu jana baada ya mchezo kujiandaa na mechi ya ligi dhidi ya Polisi utakaopigwa Jumatano na maandalizi yanaendelea vizuri,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER