Simba yailamba sukari ya Kagera Kaitaba

Timu ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Kikosi chetu kilimiliki mpira zaidi hasa kipindi cha kwanza huku tukitengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambazo nyingine tulishindwa kuzitumia.

Luis Miquissone alitupatia bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali akiwa ndani ya sita baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama aliyewapiga chenga walinzi kadhaa wa Kagera.

Chris Mugalu aliongeza la pili dakika ya 23 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Hassan Dilunga kufuatia kupiga gonga na Miquissone.

Kipindi cha pili Kocha Didier Gomez aliwatoa Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin na kuwaingiza Rally Bwalya pamoja na Medie Kagere.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 55 tukiwa nafasi ya pili huku tukiwa na michezo mitatu mkononi.

Mchezo wa mwisho katika ziara ya Kanda Ziwa utahitimishwa Jumamosi katika Uwanja wa Gwambina uliopo Misungwi tutakapokutana na Gwambina FC.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER