Simba yaifuata Namungo Ruangwa

Kikosi chetu kimeondoka leo alfajiri kuelekea Mtwara kwa ndege kabla ya kwenda Lindi kuifuata Namungo FC kikiwa na wachezaji 20 tayari kwa mchezo wa ligi kuu Jumamosi.

Simba itashuka dimbani Mei 29, mwaka huu katika Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa kuikabili Namungo kwenye mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Katika msimu huu Namungo ndiyo timu pekee ambayo hatujacheza nayo mechi yoyote ya ligi kutokana na ushiriki wetu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho.

Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na lengo letu ni lile lile kutetea ubingwa hivyo ushindi wa mchezo dhidi ya Namungo ni kipaumbele cha kwanza.

“Kikosi kimeondoka leo saa 12 asubuhi kwa ndege kuelekea Mtwara na baadae kitasafiri kwa basi hadi Lindi kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho dhidi ya Namungo.

“Malengo yetu ni kushinda kila mchezo ulio mbele yetu ili kutetea taji letu na tumejipanga kuanza mchezo wa kesho dhidi ya Namungo,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER