Simba yaifuata Kaizer Chiefs na nyota 24

Kikosi chetu kimeondoka nchini leo Jumanne Mei 11 alfajiri, kuelekea nchini Afrika Kusini tayari kwa mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs kikiwa na wachezaji wake nyota 24.

Mchezo huo wa raundi ya kwanza utapigwa Jumamosi Mei 15, mwaka huu katika Uwanja wa FNB, jijini Johannesburg kabla ya marudiano yatakayofanyika nchini wiki moja baadaye katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wote waliosafiri wamethibitika kuwa kwenye hali nzuri kiafya wakiwa wamepania kuhakikisha tunavuka kwenye hatua hii.

Kikosi Kamili kinachosafiri

Makipa
Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salim

Mabeki
Shomari Kapombe, Joash Onyango, uPascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Kennedy Juma na David Kameta.

Viungo
Jonas Mkude, Rally Bwalya, Mzamiru Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Francis Kahata na Taddeo Lwanga.

Washambuliaji
Medie Kagere, John Bocco, Ibrahim Ajib na Chris Mugalu.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. We are with our management, simba is entitled three point on Kariakoo derby for the failure young sport club to appeared on changed time for the match.Tff should not bring football politics on it.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER