Simba yaichapa Mbeya Kwanza 1-0

Kikosi chetu kimefanikiwa kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuifunga Mbeya Kwanza bao moja mtanange uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya wastani huku tukimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzitumia vizuri.

Mbeya Kwanza walicheza zaidi kwa kujilinda huku wachezaji wote wakiwa nyuma ya mpira na kufanya tuwe na kazi ngumu ya kupenya safu yao ya ulinzi.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuongeza mashambulizi langoni mwa Mbeya Kwanza lakini changamoto ikawa kumalizia nafasi.

Dakika ya 81 Clatous Chama alitupatia bao la kwanza na la pekee kwa shuti kali la chini chini baada ya kufanya shambulizi kali.

Kocha Msaidizi Seleman Matola aliwatoa John Bocco, Jonas Mkude, Rally Bwalya, Medie Kagere na Pape Sakho na kuwaingiza Chris Mugalu, Clatous Chama, Hassan Dilunga, Erasto Nyoni na Gadiel Michael.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER