Simba, yaibana FA Rabat Morocco

Kikosi chetu kimetoka sare ya mabao 2-2 na FAR Rabat katika mchezo wa kirafiki hapa nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia kutokana na timu zote kucheza soka la kasi wenyeji  walipata mabao yao kipindi cha kwanza kupitia kwa Chabani na Abba.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi kwenye lango la Rabat na kufanikiwa kusawazisha mabao yote kupitia kwa Hassan Dilunga na Pape Ousmane Sakho.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Peter Banda, Chris Mugalu, Rally Bwalya na Bernard Morrison na kuwaingiza Gadiel Michael, Saido Kanoute, Israel Patrick, Ibrahim Ajibu, Dilunga, Duncan Nyoni, Sakho na Yusuph Mhilu.

Kikosi chetu kilichoanza ni Ally Salum, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Henock Baka, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Peter Banda, Jonas Mkude, Chris Mugalu, Rally Bwalya na Jonas Mkude. Bernard Morrison

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER