Simba yafanya mazoezi ya mwisho kuivaa Dodoma

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Jamhuri.

Mchezo wa kesho ni wa pili kwetu baada ya ule wa ufunguzi dhidi ya Biashara United tuliocheza Jumatatu kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amesema tunahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo ili kurudisha ari kwa wachezaji na mashabiki.

Kapombe amesema wachezaji pia wanaumia kutokana na matokeo ambayo tumekuwa tukiyapata katika mechi zetu za karibuni na wamejipanga kuondoa hali hiyo wakianza na mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma.

“Tunahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kurudisha morali kwa wachezaji na mashabiki pia, hata wachezaji tunaumia kwa matokeo tunayopata ila muda wa kurudi kwenye nafasi yetu umewadia,” amesema Kapombe.

Hata hivyo katika mchezo wa kesho Kapombe hayupo sehemu ya kikosi kutokana na kuumia enka kwenye mechi iliopita dhidi ya Biashara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER