Simba yafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuivaa Dodoma Kesho

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa kesho wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika Viwanja vya Mo Simba Arena wachezaji wote wamehudhuria wakiwamo Joash Onyango na Taddeo Lwanga ambao walikuwa majeruhi baada ya kuumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kaizer Chiefs.

Kuelekea mchezo wa kesho wachezaji wako vizuri wakiwa na malengo yale yale ya kuingia nusu fainali kisha fainali na kutetea ubingwa.

Tukiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, tutapambana kuhakikisha tunatimiza malengo yetu ya kuchukua taji hilo na lile la Ligi Kuu ya Vodacom.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER